Zaburi 113:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema lakini anatazama chini, azione mbingu na dunia. Biblia Habari Njema - BHND lakini anatazama chini, azione mbingu na dunia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza lakini anatazama chini, azione mbingu na dunia. Neno: Bibilia Takatifu ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? Neno: Maandiko Matakatifu ambaye huinama atazame chini aone mbingu na nchi? BIBLIA KISWAHILI Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani? |
BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu.
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema BWANA; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.