Zaburi 112:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu. Biblia Habari Njema - BHND Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtu mwema huangaziwa mwanga gizani; mtu mwenye huruma, mpole na mwadilifu. Neno: Bibilia Takatifu Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. Neno: Maandiko Matakatifu Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu, yule mwenye rehema, huruma na haki. BIBLIA KISWAHILI Nuru huwaangaza wenye adili gizani; Ana fadhili na huruma na haki. |
Hapo taa yake ilipomulika juu yangu kichwani, Nami nilitembea gizani kwa njia ya mwanga wake;
Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.
na kama ukimpa mtu mwenye njaa chakula chako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu yeyote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.