Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Zaburi 112:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Biblia Habari Njema - BHND Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wazawa wake watakuwa wenye nguvu nchini; watoto wa wanyofu watapata baraka. Neno: Bibilia Takatifu Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. Neno: Maandiko Matakatifu Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi, kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa. BIBLIA KISWAHILI Wazawa wake watakuwa hodari duniani; Kizazi cha wenye adili kitabarikiwa. |
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Ikawa, baada ya kufa kwake Abrahamu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
nami nitawapa moyo mmoja na njia moja, wapate kunicha sikuzote; kwa mema yao, na ya watoto wao baada yao;
Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie.