Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana;
Zaburi 112:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Biblia Habari Njema - BHND Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Msifuni Mwenyezi-Mungu! Heri mtu anayemcha Mwenyezi-Mungu, anayefurahia sana kutii amri zake. Neno: Bibilia Takatifu Msifuni Mwenyezi Mungu. Heri mtu yule amchaye Mwenyezi Mungu, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. Neno: Maandiko Matakatifu Msifuni bwana. Heri mtu yule amchaye bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake. BIBLIA KISWAHILI Haleluya. Heri mtu yule amchaye BWANA, Apendezwaye sana na maagizo yake. |
Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana;
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.
Haleluya. Msifuni Bwana; Maana ni vema kumwimbia Mungu wetu sifa, Maana ni mwenye fadhili, na anastahili kuimbiwa sifa.
Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
Ijapokuwa mwenye dhambi amefanya maovu mara mia na akazidisha siku zake; lakini hata hivyo najua hakika ya kwamba itakuwa heri kwao wamchao Mungu, wenye kicho mbele zake;
Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.