Zaburi 111:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao. Biblia Habari Njema - BHND Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao. Neno: Bibilia Takatifu Amewaonesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine. Neno: Maandiko Matakatifu Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine. BIBLIA KISWAHILI Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. |
Wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa, Ukawakalisha wao. Wewe uliwatesa watu wa nchi, Ukawafanikisha wao.
Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.
Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia mlio wa mabaragumu hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka chini kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akisonga mbele kukabili; wakautwaa huo mji.