Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 11:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege, mpaka milimani,

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege, mpaka milimani,

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege, mpaka milimani,

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia. Unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa bwana ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 11:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Asa akamlilia BWANA, Mungu wake, akasema, BWANA, hapana kuliko wewe aliye wa kusaidia, kati yake yeye aliye hodari, na yeye asiye na nguvu; utusaidie, Ee BWANA, Mungu wetu; kwa kuwa sisi twakutegemea wewe, na kwa jina lako tumekuja juu ya jamii kubwa hii. Ee BWANA, wewe ndiwe Mungu wetu, asikushinde mwanadamu.


Je! Hao Wakushi na Walubi hawakuwa jeshi kubwa mno, wenye magari na wapanda farasi wengi sana? Lakini, kwa kuwa ulimtegemea BWANA, aliwatia mkononi mwako.


Nami nikasema, Je! Mtu kama mimi nikimbie? Naye ni nani, akiwa kama nilivyo mimi, atakayeingia hekaluni ili kuponya maisha yake? Sitaingia.


Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe.


Ee Mungu wangu, Nimekutumainia Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.


Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.


Nimemtumaini Mungu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?


BWANA, Mungu wangu, nimekukimbilia Wewe, Uniokoe na wote wanaonifuatia, uniponye.


Asije akaipapura nafsi yangu kama simba, Akaniburura hadi pasipokuwa na wa kuniponya.


Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe, Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.


Ujiponye kama paa na mkono wa mwindaji, Na kama ndege katika mkono wa mtega mitego.


Mwasemaje ninyi, Sisi tu mashujaa, watu hodari wa vita.


Saa ile ile Mafarisayo kadhaa walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.


Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.


Yonathani akampigia mtoto kelele, Haya! Hima! Usikawie. Mtoto wa Yonathani akaikusanya mishale, akaenda kwa bwana wake.


Kutoka huko Daudi akaenda Mispa ya Moabu; akamwambia mfalme wa Moabu, Tafadhali wakubalie baba yangu na mama yangu watoke huko waliko, wakakae kwenu, hata nitakapojua Mungu atakalotenda kwa ajili yangu.


Basi Daudi alikuwa akikaa nyikani ngomeni, akakaa katika nchi ya milima milima kwenye nyika ya Zifu. Naye Sauli alikuwa akimtafuta kila siku, lakini Mungu hakumtia mikononi mwake.


Ndipo Daudi aliposema moyoni mwake, Siku moja, basi, mimi nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jema zaidi kwangu kuliko kukimbia mpaka nchi ya Wafilisti; naye Sauli atakata tamaa kunihusu, asinitafute tena kote mipakani mwa Israeli; hivyo nitaokoka katika mikono yake.