Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Zaburi 109:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanasema maovu juu yangu, na kunishambulia bila kisa. Biblia Habari Njema - BHND Wanasema maovu juu yangu, na kunishambulia bila kisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanasema maovu juu yangu, na kunishambulia bila kisa. Neno: Bibilia Takatifu Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu. Neno: Maandiko Matakatifu Wamenizunguka kwa maneno ya chuki, wananishambulia bila sababu. BIBLIA KISWAHILI Naam, kwa maneno ya chuki wamenizunguka, Wamepigana nami bure. |
Absalomu alipokuwa akitoa dhabihu alituma Ahithofeli Mgiloni, Mshauri wake Daudi, aitwe kutoka mji wake, yaani, Gilo. Njama zao zikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu walizidi kuongezeka.
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Efraimu amenizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu; na Yuda hata sasa anasitasita kwa Mungu, na kwake aliye Mtakatifu, naye ni mwaminifu.
Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu?