huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Zaburi 109:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wakajue ya kuwa huu ni mkono wako; Wewe, BWANA, umeyafanya hayo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waoneshe watu kuwa ndiwe uliyetenda hayo, wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe uliyefanya hivyo. Biblia Habari Njema - BHND Waoneshe watu kuwa ndiwe uliyetenda hayo, wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe uliyefanya hivyo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waoneshe watu kuwa ndiwe uliyetenda hayo, wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ndiwe uliyefanya hivyo. Neno: Bibilia Takatifu Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee Mwenyezi Mungu, umetenda hili. Neno: Maandiko Matakatifu Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako, kwamba wewe, Ee bwana, umetenda hili. BIBLIA KISWAHILI Nao wakajue ya kuwa huu ni mkono wako; Wewe, BWANA, umeyafanya hayo. |
huyo Ezra akakwea kutoka Babeli; naye alikuwa mwandishi mwepesi katika Sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa BWANA, Mungu wa Israeli; naye mfalme akamjalia matakwa yake yote, kama mkono wa BWANA, Mungu wake, ulivyokuwa pamoja naye.
Ikawa adui zetu wote waliposikia, ndipo wamataifa wote waliotuzunguka wakaogopa, nao wakakata tamaa sana machoni pao wenyewe; maana waliitambua kazi hiyo ilivyotendwa na Mungu wetu.
Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu.
Ndipo wale waganga wakamwambia Farao, Jambo hili ni kidole cha Mungu; na moyo wake Farao ukawa mgumu asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyonena.
wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana.