Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Zaburi 109:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi ni maskini na fukara; nimejeruhiwa mpaka moyoni mwangu. Biblia Habari Njema - BHND Mimi ni maskini na fukara; nimejeruhiwa mpaka moyoni mwangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi ni maskini na fukara; nimejeruhiwa mpaka moyoni mwangu. Neno: Bibilia Takatifu Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Maana mimi ni maskini na mhitaji, moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mimi ni mnyonge na mhitaji, Na moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu. |
Naye alipofika kwa yule mtu wa Mungu kilimani, alimshika miguu. Gehazi akakaribia amwondoe; lakini mtu wa Mungu akamwambia, Mwache; maana roho yake ndani yake ina uchungu; na BWANA amenificha, wala hakuniambia.
Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo,
Nami ni maskini na mhitaji, Bwana atanitunza. Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu, Ee Mungu wangu, usikawie.
Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu.
Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.