Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Zaburi 109:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwovu huyo hakujali kabisa kuwa na huruma, ila aliwadhulumu maskini na fukara, kadhalika na watu wanyonge mpaka kifo. Biblia Habari Njema - BHND Mwovu huyo hakujali kabisa kuwa na huruma, ila aliwadhulumu maskini na fukara, kadhalika na watu wanyonge mpaka kifo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwovu huyo hakujali kabisa kuwa na huruma, ila aliwadhulumu maskini na fukara, kadhalika na watu wanyonge mpaka kifo. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo, |
Wakaambiana, Kweli sisi tulimkosea ndugu yetu, kwa kuwa tuliona shida ya roho yake, alipotusihi, wala hatukusikia, kwa hiyo shida hii imetupata.
Umeona, maana unaangalia matatizo na dhiki, Uyatwae mkononi mwako. Mtu duni hukuachia nafsi yake, Maana umekuwa msaidizi wa yatima.
Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza.
Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta, Wamwangushe chini maskini na mhitaji, Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.