na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.
Zaburi 109:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watoto wake watangetange na kuombaomba; wafukuzwe katika magofu ya nyumba zao! Biblia Habari Njema - BHND Watoto wake watangetange na kuombaomba; wafukuzwe katika magofu ya nyumba zao! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watoto wake watangetange na kuombaomba; wafukuzwe katika magofu ya nyumba zao! Neno: Bibilia Takatifu Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. Neno: Maandiko Matakatifu Watoto wake na watangetange wakiomba, na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao. BIBLIA KISWAHILI Kutanga na watange wanawe na kuomba, Watafute chakula mbali na mahame yao. |
na imwangukie Yoabu kichwani pake, na nyumba yote ya babaye, tena hiyo nyumba ya Yoabu isikose kuwa na mtu mwenye kutoka damu, au aliye na ukoma, au mwenye kutegemea fimbo, au mwenye kuanguka kwa upanga au mwenye kuhitaji chakula.
Basi ukoma wa Naamani utakushika wewe, na wazao wako hata milele. Naye akatoka usoni pake mwenye ukoma kama theluji.
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula.
Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.