Zaburi 109:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usinyamaze, ee Mungu ninayekusifu! Biblia Habari Njema - BHND Usinyamaze, ee Mungu ninayekusifu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usinyamaze, ee Mungu ninayekusifu! Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, ninayekusifu, usiwe kimya, Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, ambaye ninakusifu, usiwe kimya, BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze, |
Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
Siku nyingi nimenyamaza kimya; nimenyamaza, nikajizuia; sasa nitapiga kelele kama mwanamke aliye katika kuzaa; nitaugua na kutweta pamoja.
Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.
Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.