na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng'ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao wanaona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani.
Zaburi 107:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waliona njaa na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliona njaa na kiu; wakavunjika moyo kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Waliona njaa na kiu; wakavunjika moyo kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliona njaa na kiu; wakavunjika moyo kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika. Neno: Maandiko Matakatifu Walikuwa na njaa na kiu, nafsi zao zikadhoofika. BIBLIA KISWAHILI Waliona njaa na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. |
na asali, na siagi, na kondoo, na samli ya ng'ombe, wapate kula Daudi na watu waliokuwa pamoja naye; kwani walisema, Watu hao wanaona njaa, tena wamechoka, nao wana kiu huku nyikani.
wana wa Israeli wakawaambia, Laiti tungalikufa kwa mkono wa BWANA katika nchi ya Misri, hapo tulipoketi karibu na zile sufuria za nyama, tulipokula vyakula hata kushiba; kwani mmetutoa huko na kututia katika bara hii, ili kutuua kwa njaa kusanyiko hili lote.
Watu wakawa na kiu huko; nao wakamnung'unikia Musa, wakasema, Mbona umetupandisha kutoka Misri, kutuua sisi na watoto wetu na wanyama wetu kwa kiu?
Mfua chuma hufanza shoka, hufanya kazi kwa makaa, huitengeneza sanamu kwa nyundo, huifanyiza kwa nguvu za mkono wake; naam, huona njaa, nguvu zake zikampungukia; asipokunywa maji huzimia.
Nikitoka kwenda shambani, tazama, wako huko waliouawa kwa upanga! Na nikiingia mjini, tazama, wamo humo wanaougua kwa sababu ya njaa! Maana nabii na kuhani, wote wawili, huenda huku na huko katika nchi, wala hawana maarifa.
Inuka, ulalamike usiku, Mwanzo wa mikesha yake; Mimina moyo wako kama maji usoni pa Bwana; Umwinulie mikono yako; Kwa uhai wa watoto wako wachanga wazimiao kwa njaa, Mwanzo wa kila njia kuu.