Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Zaburi 107:33 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amegeuza mito ikawa jangwa, Na chemchemi za maji zikawa nchi kavu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu aliigeuza mito kuwa jangwa, chemchemi akazikausha kabisa. Biblia Habari Njema - BHND Mungu aliigeuza mito kuwa jangwa, chemchemi akazikausha kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu aliigeuza mito kuwa jangwa, chemchemi akazikausha kabisa. Neno: Bibilia Takatifu Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zinazotiririka kuwa ardhi yenye kiu, Neno: Maandiko Matakatifu Yeye aligeuza mito kuwa jangwa, chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu, BIBLIA KISWAHILI Amegeuza mito ikawa jangwa, Na chemchemi za maji zikawa nchi kavu. |
Ahabu akamwambia Obadia, Pita katika nchi, kwenye chemchemi zote za maji, na vijito vyote; labda tutapata majani, tuwahifadhi hai farasi na nyumbu, tusipate hasara ya hao wanyama wote.
Nitaharibu milima na vilima, nitavikausha vyote vimeavyo; nitaifanya mito ya maji kuwa visiwa, na kuyakausha maziwa ya maji.
Basi, nilipokuja, mbona hapakuwa na mtu? Nilipoita, mbona hapakuwa na mtu aliyenijibu? Je! Mkono wangu ni mfupi, hata nisiweze kukomboa? Au je! Mimi sina nguvu za kuponya? Tazama, kwa kukemea kwangu naikausha bahari, mito ya maji naifanya kuwa jangwa; samaki wao wanuka kwa sababu hapana maji, nao wafa kwa kiu.
Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji; Nao hufika visimani wasipate maji; Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.
Nami nitaikausha mito, na kuiuza nchi, na kuitia katika mikono ya watu wabaya; nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, na watu wote walio ndani yake, kwa mkono wa wageni; mimi, BWANA, nimenena neno hili.
Naam, hata wanyama pori wanakulilia wewe; Kwa maana vijito vya maji vimekauka, Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.
Yeye huikemea bahari na kuikausha, pia huikausha mito yote; Bashani hulegea, na Karmeli; nalo ua la Lebanoni hulegea.
Naye atanyosha mkono wake juu ya upande wa kaskazini, na kuiangamiza Ashuru; naye ataufanya Ninawi kuwa ukiwa, kuwa mahali pakavu kama jangwa.
Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.