Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Zaburi 107:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wamtukuze katika kusanyiko la watu, Na wamhimidi katika baraza la wazee. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mtukuzeni katika kusanyiko la watu, na kumsifu katika baraza la wazee. Biblia Habari Njema - BHND Mtukuzeni katika kusanyiko la watu, na kumsifu katika baraza la wazee. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mtukuzeni katika kusanyiko la watu, na kumsifu katika baraza la wazee. Neno: Bibilia Takatifu Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee. Neno: Maandiko Matakatifu Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu, na wamsifu katika baraza la wazee. BIBLIA KISWAHILI Na wamtukuze katika kusanyiko la watu, Na wamhimidi katika baraza la wazee. |
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Kwako zinatoka sifa zangu Katika kusanyiko kubwa. Nitaziondoa nadhiri zangu Mbele yao wamchao.
Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu; Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu; Maana BWANA, Mungu wetu, ni mtakatifu.
BWANA ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza.
Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
Ee BWANA, wewe u Mungu wangu; Nitakutukuza na kulihimidi jina lako; Kwa kuwa umetenda mambo ya ajabu, Mashauri ya kale, kwa uaminifu na kweli.