Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 107:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa, wala pasiwe na wa kuwasaidia.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Walikuwa hoi kwa kazi ngumu, wakaanguka chini, pasiwe na wa kuwasaidia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Walikuwa hoi kwa kazi ngumu, wakaanguka chini, pasiwe na wa kuwasaidia.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Walikuwa hoi kwa kazi ngumu, wakaanguka chini, pasiwe na wa kuwasaidia.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwa na mtu wa kuwasaidia.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Aliwatumikisha kwa kazi ngumu; walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hata akawadhili moyo kwa taabu, Wakajikwaa, wala pasiwe na wa kuwasaidia.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 107:12
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kwani BWANA akayaona mateso ya Israeli, kwamba yalikuwa machungu sana; maana hakukuwa na mfungwa wala asiyefungwa, wala msaidizi kwa ajili ya Israeli.


Hata alipokuwa katika kusema nao, tazama, yule aliyetumwa akamshukia; naye akasema, Angalia, mabaya haya yatoka kwa BWANA; kwani mimi kumngojea BWANA tena?


Nayo yawapatia faida nyingi wafalme uliowaweka kututawala kwa sababu ya dhambi zetu; tena wana mamlaka juu ya miili yetu, na juu ya wanyama wetu, kadiri wapendavyo, nasi tuko katika dhiki kuu.


Mungu haondoi hasira zake; Hao wamsaidiao Rahabu huinama chini yake.


Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.


Usiwe mbali nami maana taabu i karibu, Kwa maana hakuna msaidizi.


Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.


nami nitalitia mikononi mwao wakutesao; waliokuambia nafsi yako, Inama, tupate kupita; nawe uliufanya mgongo wako kuwa kama nchi, na kama njia, kwa hao wapitao juu yake.


Basi sasa, nafanya nini hapa, asema BWANA, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure? Hao wanaowatawala wanapiga yowe, asema BWANA, na jina langu linatukanwa daima mchana kutwa.


Nikatazama, wala hapakuwa na wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.


Wafilisti wakamkamata, wakamng'oa macho; wakateremka naye mpaka Gaza, wakamfunga kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga ngano katika gereza.


Samsoni akasema; Na nife pamoja na hawa Wafilisti. Akainama kwa nguvu zake zote; ile nyumba ikawaangukia hao wakuu, na watu wote waliokuwa ndani yake. Basi wale watu aliowaua wakati wa kufa kwake walikuwa wengi kuliko wale aliowaua wakati wa uhai wake.