basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao.
Zaburi 106:44 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo Mungu alizijali taabu zao, wakati aliposikia kilio chao; Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo Mungu alizijali taabu zao, wakati aliposikia kilio chao; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo Mungu alizijali taabu zao, wakati aliposikia kilio chao; Neno: Bibilia Takatifu Lakini akaangalia mateso yao aliposikia kilio chao; Neno: Maandiko Matakatifu Lakini akaangalia mateso yao wakati aliposikia kilio chao; BIBLIA KISWAHILI Lakini aliyaangalia mateso yao, Aliposikia kilio chao. |
basi usikie huko mbinguni, ukaisamehe dhambi ya watu wako Israeli, na kuwarejeza tena katika nchi uliyowapa wao na baba zao.
Na kila wakati BWANA alipowainulia waamuzi, ndipo BWANA alikuwa pamoja na mwamuzi huyo, akawaokoa na mikono ya adui zao siku zote za mwamuzi huyo; maana BWANA alisikitishwa na kilio chao kwa sababu ya watu wale waliowaonea na kuwasumbua.
Kisha wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia wana wa Israeli mwokozi, aliyewaokoa, yaani, Othnieli mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu.
Wana wa Israeli wakamlilia BWANA; kwa kuwa Sisera alikuwa na magari ya chuma mia tisa ya vita; naye akawakandamiza sana wana wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikia.