Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya BWANA, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine.
Zaburi 106:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waliabudu sanamu za miungu yao, nazo zikawa mtego wa kuwaangamiza. Biblia Habari Njema - BHND Waliabudu sanamu za miungu yao, nazo zikawa mtego wa kuwaangamiza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waliabudu sanamu za miungu yao, nazo zikawa mtego wa kuwaangamiza. Neno: Bibilia Takatifu Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. Neno: Maandiko Matakatifu Waliabudu sanamu zao, zikawa mtego kwao. BIBLIA KISWAHILI Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao. |
Yalitukia hayo kwa sababu wana wa Israeli walikuwa wametenda dhambi juu ya BWANA, Mungu wao, aliyewaleta kutoka katika nchi ya Misri watoke chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri, wakawaacha miungu mingine.
Wasikae katika nchi yako, wasije wakakufanya kunitendea mimi dhambi; kwa sababu ukiitumikia miungu yao, jambo hili halikosi litakuwa ni (mtego) tanzi kwako.
Ndipo watakaposema watu, Ni kwa kuwa waliacha agano la BWANA, Mungu wa baba zao, alilofanya nao hapo alipowatoa katika nchi ya Misri;
Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.
jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.
Kisha wana wa Israeli walifanya tena yaliyo maovu mbele za macho ya BWANA, wakawatumikia Mabaali, na Maashtorethi, na miungu ya Shamu, na miungu ya Sidoni, na miungu ya Moabu, na miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti; nao wakamuacha BWANA, wala hawakumtumikia yeye.
Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za BWANA bali wao hawakufanya hivyo.
Lakini ikawa, wakati alipokufa mwamuzi huyo, wakarudi nyuma wakafanya maovu kuliko baba zao, kwa kuifuata miungu mingine ili kuitumikia, na kuinama mbele yao; hawakuacha matendo yao, wala njia zao za ukaidi.
Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni mtego kwenu.