Zaburi 106:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyetenda mambo makuu nchini Misri, Biblia Habari Njema - BHND Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyetenda mambo makuu nchini Misri, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyetenda mambo makuu nchini Misri, Neno: Bibilia Takatifu Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyetenda mambo makuu huko Misri, Neno: Maandiko Matakatifu Walimsahau Mungu aliyewaokoa, aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri, BIBLIA KISWAHILI Wakamsahau Mungu, mwokozi wao, Aliyetenda makuu katika Misri. |
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
Maana umemsahau Mungu wa wokovu wako, wala hukuukumbuka mwamba wa ngome yako; kwa sababu hiyo ulipanda mashamba yapendezayo, na kutia ndani yake mizabibu migeni.
Hubirini, toeni habari; naam, na wafanye mashauri pamoja; ni nani aliyeonesha haya tangu zamani za kale? Ni nani aliyeyahubiri hapo zamani? Si mimi, BWANA? Wala hapana Mungu zaidi ya mimi; Mungu mwenye haki, mwokozi; hapana mwingine zaidi ya mimi.
Je! Mwanamwali aweza kusahau mapambo yake, au bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa muda wa siku zisizo na hesabu.
Lakini nitairehemu nyumba ya Yuda; nitawaokoa kwa BWANA, Mungu wao; wala sitawaokoa kwa upinde, wala kwa upanga, wala kwa silaha, wala kwa farasi, wala kwa wapanda farasi.
Yeye ndiye fahari yako, na yeye ndiye Mungu wako, aliyekutendea mambo haya makubwa, ya kutisha, uliyoyaona kwa macho yako.
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?
BWANA akaonesha ishara na maajabu makubwa na mazito, juu ya Misri, Farao, na nyumba yake yote, mbele ya macho yetu;
akalifunua neno lake kwa majira yake katika ule ujumbe niliokabidhiwa kwa amri ya Mwokozi wetu Mungu;
wasiwe wezi; bali wauoneshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mungu aliye Mwokozi wetu katika mambo yote.
Kwani wana wa Israeli hawakumkumbuka BWANA, Mungu wao, ambaye ndiye aliyewaokoa na mikono ya adui zao wote pande zote;