Zaburi 106:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Bali walitamani sana nyikani, Wakamjaribu Mungu jangwani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani, wakamjaribu Mungu kule nyikani. Biblia Habari Njema - BHND Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani, wakamjaribu Mungu kule nyikani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Walijawa na tamaa kubwa kule jangwani, wakamjaribu Mungu kule nyikani. Neno: Bibilia Takatifu Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. Neno: Maandiko Matakatifu Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. BIBLIA KISWAHILI Bali walitamani sana nyikani, Wakamjaribu Mungu jangwani. |
Kwa hiyo hao watu wakamgombeza Musa, wakasema, Tupe maji tunywe. Musa akawaambia, Kwa nini mnanigombeza? Mbona mnamjaribu BWANA?
Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, Ni nani atakayetupa nyama tule?
kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;
Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.