Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Zaburi 105:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Hukumu zake ziko duniani kote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye ndiye Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; hukumu zake zina nguvu duniani kote. Biblia Habari Njema - BHND Yeye ndiye Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; hukumu zake zina nguvu duniani kote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye ndiye Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu; hukumu zake zina nguvu duniani kote. Neno: Bibilia Takatifu Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, hukumu zake ziko duniani kote. Neno: Maandiko Matakatifu Yeye ndiye bwana Mwenyezi Mungu wetu, hukumu zake zimo duniani pote. BIBLIA KISWAHILI Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu; Hukumu zake ziko duniani kote. |
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.