Zaburi 105:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya, Miujiza yake na hukumu alizotoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, miujiza yake na hukumu alizotoa, Biblia Habari Njema - BHND Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, miujiza yake na hukumu alizotoa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, miujiza yake na hukumu alizotoa, Neno: Bibilia Takatifu Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, Neno: Maandiko Matakatifu Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, BIBLIA KISWAHILI Yakumbukeni matendo yake ya ajabu aliyoyafanya, Miujiza yake na hukumu alizotoa. |
Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi Miujiza yako na mawazo yako kwetu; Hakuna awezaye kufananishwa nawe; Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri, Ni mengi sana hayahesabiki.
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.
Kumbuka siku za kale, Tafakari miaka ya vizazi vingi; Mwulize baba yako, naye atakuonesha; Wazee wako, nao watakuambia.
Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza miaka hii arubaini katika jangwa, ili akunyenyekeze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo.
Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.