na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Zaburi 105:44 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliwapa nchi za mataifa mengine na kuwakabidhi mashamba ya wenyeji; Biblia Habari Njema - BHND Aliwapa nchi za mataifa mengine na kuwakabidhi mashamba ya wenyeji; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliwapa nchi za mataifa mengine na kuwakabidhi mashamba ya wenyeji; Neno: Bibilia Takatifu akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali ambayo wengine walikuwa wameitaabikia: Neno: Maandiko Matakatifu akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi wa mali wengine walikuwa wameitaabikia: BIBLIA KISWAHILI Akawapa nchi za mataifa, wakairithi kazi ya watu; |
na sheria, na hukumu, na torati, na amri, alizowaandikia, hizo ndizo mtakazozishika na kuzifanya hata milele; wala msiche miungu mingine.
Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha makabila ya Israeli katika hema zao.
nao wakaingia, wakaimiliki; lakini hawakuitii sauti yako, wala hawakuenda katika sheria yako; hawakutenda neno lolote katika haya uliyowaagiza wayatende; basi, kwa sababu hii umeleta juu yao mabaya haya yote;
Basi Yoshua akaitwaa hiyo nchi yote, sawasawa na hayo yote BWANA aliyokuwa amemwambia Musa; Yoshua naye akawapa Israeli kuwa ni urithi wao, sawasawa na walivyogawanyikana kwa makabila yao. Kisha nchi ikatulia isiwe na vita tena.
Basi BWANA aliwapa Israeli nchi hiyo yote, ambayo aliapa kwamba atawapa baba zao; nao wakaimiliki, na kukaa humo.
Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa makabila yenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa magharibi.
Nami nimewapa ninyi nchi msiyoitendea kazi, na miji msiyoijenga, nanyi mmekaa humo; mnakula matunda ya mashamba ya mizabibu na mizeituni msiyoipanda.
Kisha nikawaleta na kuwaingiza katika nchi ya Waamori waliokaa ng'ambo ya pili ya Yordani; nao wakapigana nanyi; nikawatia mikononi mwenu, mkaimiliki nchi yao; nami nikawaangamiza mbele yenu.
Nao wakala katika mazao ya nchi siku ya pili ya kuiandama hiyo sikukuu ya Pasaka, mikate isiyotiwa chachu, na bisi, siku iyo hiyo.