Zaburi 105:43 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi akawatoa watu wake nchini, wateule wake wakaimba na kushangilia. Biblia Habari Njema - BHND Basi akawatoa watu wake nchini, wateule wake wakaimba na kushangilia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi akawatoa watu wake nchini, wateule wake wakaimba na kushangilia. Neno: Bibilia Takatifu Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe, Neno: Maandiko Matakatifu Aliwatoa watu wake kwa furaha, wateule wake kwa kelele za shangwe, BIBLIA KISWAHILI Akawatoa watu wake kwa shangwe, Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. |
Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.
Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa jeuri.
Na hao waliokombolewa na BWANA watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitatoweka.
Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya shambani itapiga makofi.
Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza.
Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika Bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arubaini.
Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi.
nami niliwaokoa na mikono ya Wamisri, na mikono ya wote waliokuwa wakiwaonea, nami niliwafukuza watoke mbele zenu, nami niliwapa ninyi nchi yao;