BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Zaburi 105:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Abrahamu, mtumishi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. Biblia Habari Njema - BHND Aliikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Abrahamu mtumishi wake. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Ibrahimu mtumishi wake. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu, aliyompa Ibrahimu mtumishi wake. BIBLIA KISWAHILI Maana alilikumbuka neno lake takatifu, Na Abrahamu, mtumishi wake. |
BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.
Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Abrahamu na Isaka na Yakobo.
Mkumbuke Abrahamu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.
Wewe utamtimilizia Yakobo kweli yako, na Abrahamu rehema zako, ulizowaapia baba zetu tangu siku za kale.
Wakumbuke watumishi wako, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; usiangalie ukaidi wa watu hawa, wala uovu wao, wala dhambi yao;
Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.