Zaidi ya hayo ukawaongoza kwa nguzo ya wingu mchana; na kwa nguzo ya moto usiku; ili kuwapa mwanga katika njia iliyowapasa kuiendea.
Zaburi 105:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mungu alitandaza wingu juu ya watu wake, na moto ili kuwaangazia usiku. Biblia Habari Njema - BHND Mungu alitandaza wingu juu ya watu wake, na moto ili kuwaangazia usiku. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mungu alitandaza wingu juu ya watu wake, na moto ili kuwaangazia usiku. Neno: Bibilia Takatifu Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku. Neno: Maandiko Matakatifu Alitandaza wingu kama kifuniko, na moto kuwamulikia usiku. BIBLIA KISWAHILI Alitandaza wingu liwe kifuniko, Na moto ili uwaangazie usiku. |
Zaidi ya hayo ukawaongoza kwa nguzo ya wingu mchana; na kwa nguzo ya moto usiku; ili kuwapa mwanga katika njia iliyowapasa kuiendea.
hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; nguzo ya wingu haikuondoka kwao wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala nguzo ya moto haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonesha njia watakayoiendea.
Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri.
Tena juu ya makao yote ya mlima Sayuni, na juu ya makusanyiko yake, BWANA ataumba wingu na moshi wakati wa mchana, na mwangaza wa miali ya moto wakati wa usiku; kwa maana juu ya utukufu wote itatandazwa sitara.