Zaburi 105:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kisha akamtuma Mose mtumishi wake, akamtuma na Aroni mteule wake. Biblia Habari Njema - BHND Kisha akamtuma Mose mtumishi wake, akamtuma na Aroni mteule wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kisha akamtuma Mose mtumishi wake, akamtuma na Aroni mteule wake. Neno: Bibilia Takatifu Akamtuma Musa mtumishi wake, pamoja na Haruni, aliyemchagua. Neno: Maandiko Matakatifu Akamtuma Musa mtumishi wake, pamoja na Haruni, aliyemchagua. BIBLIA KISWAHILI Akamtuma Musa, mtumishi wake, Na Haruni ambaye amemchagua. |
Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua majina yao mbele za BWANA juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.
Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.
BWANA akamwambia Haruni, Nenda jangwani uonane na Musa. Naye akaenda, akamkuta katika mlima wa Mungu, akambusu.
Ingia ndani, ukaseme na Farao, mfalme wa Misri, ili awape ruhusa wana wa Israeli watoke nchi yake.
BWANA akamwambia Musa, Angalia, nimekufanya wewe kuwa kama Mungu kwa Farao; na huyo ndugu yako Haruni atakuwa nabii wako.
Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao.
Kwa maana nilikupandisha kutoka nchi ya Misri, na kukukomboa utoke katika nyumba ya utumwa, nami niliwatuma Musa, na Haruni, na Miriamu, watangulie mbele yako.
viwe ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili mgeni yeyote asiye wa kizazi cha Haruni, asikaribie kufukiza uvumba mbele za BWANA; asiwe mfano wa Kora, na mkutano wake; kama BWANA alivyonena naye, kwa kupitia kwa Musa.
Kisha nikawatuma Musa na Haruni nikaipiga nchi ya Misri, kwa hayo yote niliyoyatenda kati yake; hatimaye nikawatoa ninyi.
Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.