BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa kwa muda wa miaka mia nne.
Zaburi 105:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliwafanya Wamisri wawachukie watu wake, wakawatendea hila watumishi wake. Biblia Habari Njema - BHND Aliwafanya Wamisri wawachukie watu wake, wakawatendea hila watumishi wake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliwafanya Wamisri wawachukie watu wake, wakawatendea hila watumishi wake. Neno: Bibilia Takatifu Aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. Neno: Maandiko Matakatifu ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake, wakatenda hila dhidi ya watumishi wake. BIBLIA KISWAHILI Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake. |
BWANA akamwambia Abramu, Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake, watawatumikia watu wale, nao watateswa kwa muda wa miaka mia nne.
akasema, Wakati mnapowazalisha wanawake wa Kiebrania na kuona kuwa ni mtoto wa kiume basi mwueni, bali ikiwa ni mtoto wa kike, na aishi.
BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionesha ishara zangu hizi kati yao;
Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.
lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.
Huyo akawafanyia hila kabila yetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru wawatupe watoto wao wachanga, ili wasiishi.
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.