Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Zaburi 103:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Biblia Habari Njema - BHND Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu! Usisahau kamwe wema wake wote. Neno: Bibilia Takatifu Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu, wala usisahau wema wake wote: Neno: Maandiko Matakatifu Ee nafsi yangu, umhimidi bwana, wala usisahau wema wake wote, BIBLIA KISWAHILI Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote. |
Walakini Hezekia hakuwa na shukrani kadiri alivyofadhiliwa; kwa kuwa moyo wake ulijawa na kiburi; kwa hiyo ikawako hasira juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu.
Baba zetu katika Misri Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.
Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.
Je! Mnamlipa BWANA hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
Kwa sababu wakuu walitangulia katika Israeli, Kwa sababu watu walijitoa nafsi zao kwa hiari yao, Mhimidini BWANA.
Moyo wangu unawaelekea makamanda wa Israeli, Waliojitoa nafsi zao kwa hiari yao miongoni mwa watu; Mhimidini BWANA.