Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Zaburi 103:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Biblia Habari Njema - BHND Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu; nafsi yangu yote ilisifu jina lake takatifu! Neno: Bibilia Takatifu Ee nafsi yangu, umhimidi Mwenyezi Mungu. Vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Neno: Maandiko Matakatifu Ee nafsi yangu, umhimidi bwana. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. BIBLIA KISWAHILI Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. |
Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Wewe, BWANA, Mungu wangu, Umejifanya mkuu sana; Umejivika heshima na utukufu.
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono; Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
Imekuwaje, basi? Nitaomba kwa roho, tena nitaomba kwa akili pia; nitaimba kwa roho, tena nitaimba kwa akili pia.
Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Na hawa wenye uhai wanne, kila mmoja alikuwa na mabawa sita; pande zote na ndani wamejaa macho, wala hawapumziki mchana wala usiku, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Bwana Mungu Mwenyezi, aliyekuwako na aliyeko na atakayekuja.