Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.
Zaburi 102:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana ninakula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Biblia Habari Njema - BHND Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Majivu yamekuwa chakula changu, machozi nayachanganya na kinywaji changu, Neno: Bibilia Takatifu Ninakula majivu kama chakula changu, nimechanganya kinywaji changu na machozi Neno: Maandiko Matakatifu Ninakula majivu kama chakula changu na nimechanganya kinywaji changu na machozi BIBLIA KISWAHILI Maana ninakula majivu kama chakula, Na kukichanganya kinywaji changu na machozi. |
Kwani kuugua kwangu kwaja kana kwamba ni chakula, Na kunguruma kwangu kumemiminika kama maji.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Hula majivu; moyo uliodanganyika umempotosha, asiweze kuiokoa nafsi yake, wala kusema, Je! Sio uongo mkononi mwangu?
Watayaramba mavumbi kama nyoka, kama vitu vitambaavyo juu ya nchi watatoka katika mahali walimojificha, wakitetemeka; watakuja kwa BWANA, Mungu wetu, kwa hofu, nao wataogopa kwa sababu yako.