Nao wazee wa nyumba yake wakaondoka, wakasimama karibu naye, ili wamwinue kutoka chini; lakini hakukubali, wala hakula chakula pamoja nao.
Zaburi 102:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula. Biblia Habari Njema - BHND Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimepondwa moyoni kama nyasi na kunyauka; sina hata hamu ya chakula. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani; ninasahau kula chakula changu. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani, ninasahau kula chakula changu. BIBLIA KISWAHILI Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu. |
Nao wazee wa nyumba yake wakaondoka, wakasimama karibu naye, ili wamwinue kutoka chini; lakini hakukubali, wala hakula chakula pamoja nao.
Kisha Ezra akaondoka hapo mbele ya nyumba ya Mungu, akaingia katika chumba cha Yehohanani, mwana wa Eliashibu; hata, alipofika huko, hakula mkate, wala hakunywa maji; kwa maana alilia kwa sababu ya kosa lile la watu wa uhamisho.
Nayachukia maisha yangu; Nitayasema malalamiko yangu wazi; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Nafsi yangu imeinama ndani yangu, kwa hiyo nitakukumbuka, Toka nchi ya Yordani, na Mahermoni, na toka kilima cha Mizari.
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Majani yakauka, ua lanyauka; Kwa sababu pumzi ya BWANA yapita juu yake. Hakika watu ni majani.