Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
Zaburi 102:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu, na kilio changu kikufikie. Biblia Habari Njema - BHND Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu, na kilio changu kikufikie. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu, na kilio changu kikufikie. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, usikie maombi yangu; kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, usikie maombi yangu, kilio changu cha kuomba msaada kikufikie. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, usikie kuomba kwangu, Kilio changu kikufikie. |
Ndipo wakasimama makuhani Walawi, wakawabariki watu; ikasikiwa sauti yao, sala yao ikafika hata makao yake matakatifu, yaani, mbinguni.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Katika shida yangu nilimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
Ee BWANA, usikie maombi yangu, Utege sikio lako niliapo, Usiyapuuze machozi yangu. Kwa maana mimi ni mgeni wako, Msafiri kama baba zangu wote.
Nayakumbuka mambo haya kwa uchungu moyoni mwangu, Jinsi nilivyokuwa nikienda na mkutano, Na kuwaongoza hadi katika nyumba ya Mungu, Kwa sauti ya furaha na kusifu, mkutano wa sikukuu.
Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.
Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo, Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
Na kisha baada ya muda, yule mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;
Nao wakaiondoa hiyo miungu ya kigeni iliyokuwa kati yao, nao wakamtumikia BWANA; na roho yake ilihuzunika kwa sababu ya msiba wa Israeli.
Kesho, wakati kama huu, nitakuletea mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe mtie mafuta ili awe mkuu juu ya watu wangu Israeli, naye atawaokoa watu wangu na mikono ya Wafilisti; maana nimewaangalia watu wangu, kwa sababu kilio chao kimenifikia.