Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
Zaburi 101:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kila asubuhi nitawaangamiza Waovu wote nchini. Nikiwatenga wote watendao uovu Na mji wa BWANA. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku kwa siku nitawaangamiza waovu wote nchini; nitawaangamiza wabaya wote mjini mwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Siku kwa siku nitawaangamiza waovu wote nchini; nitawaangamiza wabaya wote mjini mwa Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku kwa siku nitawaangamiza waovu wote nchini; nitawaangamiza wabaya wote mjini mwa Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda maovu kutoka mji wa Mwenyezi Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kila asubuhi nitawanyamazisha waovu wote katika nchi; nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya kutoka mji wa bwana. BIBLIA KISWAHILI Kila asubuhi nitawaangamiza Waovu wote nchini. Nikiwatenga wote watendao uovu Na mji wa BWANA. |
Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.
Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa BWANA wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha hata milele.
Mfalme mwenye hekima huwapepeta wasio haki; Naye hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
Ee nyumba ya Daudi, BWANA asema hivi, Hukumuni hukumu ya haki asubuhi, mkawaponye waliotekwa nyara na mkono wake aliyewadhulumu, ghadhabu yangu isije ikatoka kama moto, ikaunguza, asiweze mtu yeyote kuuzima, kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
Hawatakaa katika nchi ya BWANA; lakini Efraimu atarudi Misri, nao watakula chakula najisi katika Ashuru.
Sikieni haya, tafadhali, enyi vichwa vya nyumba ya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli, mnaochukia hukumu, na kuipotosha adili.
Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo.