Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo,
Zaburi 10:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa kiburi waovu wanawatesa maskini; njama zao ziwanase wao wenyewe. Biblia Habari Njema - BHND Kwa kiburi waovu wanawatesa maskini; njama zao ziwanase wao wenyewe. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa kiburi waovu wanawatesa maskini; njama zao ziwanase wao wenyewe. Neno: Bibilia Takatifu Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. Neno: Maandiko Matakatifu Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini, waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga. BIBLIA KISWAHILI Kwa kiburi chake asiye haki mnyonge anafuatiwa kwa ukali; Na wanaswe kwa hila zizo hizo walizoziwaza. |
Kwa kuwa hakukumbuka kutenda fadhili, Bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, Hata akamwua mtu aliyevunjika moyo,
Wenye kiburi wamenifichia mtego na kamba; Wametandika wavu kando ya njia; Wameniwekea matanzi.
Midomo ya uongo iwe na ububu, Imneneayo mwenye haki maneno ya kiburi, Kwa majivuno na dharau.
Kwa dhambi ya kinywa chao, Na kwa neno la midomo yao, Wanaswe kwa kiburi chao, Kwa ajili ya kulaani na uongo wasemao.
Sasa najua ya kuwa BWANA ni mkuu kuliko miungu yote; naam, katika jambo hilo walilowatenda kwa ujeuri.
Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
Wao wakuonao watakukazia macho, Watakuangalia sana, wakisema, Je! Huyu ndiye aliyeitetemesha dunia, Huyu ndiye aliyetikisa falme;
ndipo Azaria, mwana wa Hoshaya, na Yohana mwana wa Karea, na watu wote wenye kiburi wakanena, wakimwambia Yeremia, Unasema uongo; BWANA, Mungu wetu, hakukutuma useme, Msiende Misri kukaa huko;