Zaburi 10:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Inuka, Ee Mungu BWANA, uuinue mkono wako, Ee Mungu Usiwasahau wanyonge. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inuka, ee Mwenyezi-Mungu, uwaadhibu; usiwasahau wanaodhulumiwa. Biblia Habari Njema - BHND Inuka, ee Mwenyezi-Mungu, uwaadhibu; usiwasahau wanaodhulumiwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inuka, ee Mwenyezi-Mungu, uwaadhibu; usiwasahau wanaodhulumiwa. Neno: Bibilia Takatifu Inuka Mwenyezi Mungu! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge. Neno: Maandiko Matakatifu Inuka bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu. Usiwasahau wanyonge. BIBLIA KISWAHILI Inuka, Ee Mungu BWANA, uuinue mkono wako, Ee Mungu Usiwasahau wanyonge. |
Inuka, Ee BWANA, umkabili, umwangushe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi yangu na mtu mbaya.
Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kulia Uwaokoe kutoka kwa adui zao.
BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe, Maana umewapiga taya adui zangu wote; Umewavunja meno wasio haki.
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Wewe, BWANA, unifadhili, Tazama mateso niteswayo na wanaonichukia; Wewe uniinuaye katika malango ya mauti,
BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.
Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, nikumbuke nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.