Zaburi 1:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi. Biblia Habari Njema - BHND Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Mwenyezi-Mungu huziongoza njia za waadilifu; lakini njia za waovu zitaishia katika maangamizi. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki, bali njia za waovu zitaangamia. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana bwana huziangalia njia za mwenye haki, bali njia ya waovu itaangamia. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki, Bali njia ya wasio haki itapotea. |
Asiye haki ataona na kusikitika, Atasaga meno yake na kuondoka, Matumaini ya wasio haki hupotea.
Utazame mkono wangu wa kulia ukaone, Kwa maana sina mtu anijuaye. Makimbilio yamenipotea, Hakuna wa kunitunza roho.
BWANA huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huiharibu.
Adui wameangamia na kuwa magofu milele. Nayo miji yao uliing'oa; Hata kumbukumbu lao limepotea.
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
Lakini hao kama wanyama wasio na akili, ambao walizaliwa kama wanyama tu wa kukamatwa na kupotezwa, wakikufuru katika mambo wasiyoyajua, wataangamizwa katika maangamizo yao;
Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake; Bali waovu watanyamazishwa gizani, Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;