Yoshua 8:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Isipokuwa mifugo na nyara za mji Israeli wakatwaa wenyewe kuwa ni mapato yao, sawasawa na hilo neno la BWANA alilomwamuru Yoshua. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waisraeli waliteka tu wanyama na mali kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Biblia Habari Njema - BHND Waisraeli waliteka tu wanyama na mali kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waisraeli waliteka tu wanyama na mali kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Yoshua. Neno: Bibilia Takatifu Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vile Mwenyezi Mungu alivyokuwa amemwamuru Yoshua. Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Israeli wakajichukulia mifugo na nyara za mji huu, kama vile bwana alivyokuwa amemwagiza Yoshua. BIBLIA KISWAHILI Isipokuwa mifugo na nyara za mji Israeli wakatwaa wenyewe kuwa ni mapato yao, sawasawa na hilo neno la BWANA alilomwamuru Yoshua. |
Fanya jumla ya hayo mateka ya wanadamu, na ya wanyama pia, wewe, na Eleazari kuhani, na wakuu wa nyumba za baba za mkutano;
Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema?
Nao wakatoka nje, wao na mjeshi yao yote pamoja nao, watu wengi mno, kama mchanga ulio ufuoni mwa bahari kwa wingi, pamoja na farasi na magari mengi sana.
nawe utautenda mji wa Ai na mfalme wake kama ulivyoutenda mji wa Yeriko na mfalme wake; lakini nyara zake na wanyama wake wa mji mtavitwaa kuwa mateka yenu wenyewe; huo mji uuwekee waoteaji upande wa nyuma.
Basi Yoshua akauteketeza mji wa Ai, na kuufanya kuwa ni rundo la magofu hata milele, kuwa ni ukiwa hata siku hii ya leo.