Yusufu Akakaa katika Misri, yeye na nyumba ya baba yake. Yusufu Akaishi miaka mia moja na kumi.
Yoshua 24:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, mwenye umri wa miaka mia moja na kumi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baada ya mambo hayo, Yoshua, mwana wa Nuni na mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, akafariki akiwa na umri wa miaka 110. Biblia Habari Njema - BHND Baada ya mambo hayo, Yoshua, mwana wa Nuni na mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, akafariki akiwa na umri wa miaka 110. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baada ya mambo hayo, Yoshua, mwana wa Nuni na mtumishi wa Mwenyezi-Mungu, akafariki akiwa na umri wa miaka 110. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Mwenyezi Mungu akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa bwana akafa akiwa na umri wa miaka mia moja na kumi. BIBLIA KISWAHILI Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, mwenye umri wa miaka mia moja na kumi. |
Yusufu Akakaa katika Misri, yeye na nyumba ya baba yake. Yusufu Akaishi miaka mia moja na kumi.
Basi Yusufu akafa, mwenye miaka mia moja na kumi; wakampaka dawa, wakamtia katika sanduku, huko Misri.
Wakamzika katika nchi ya urithi wake, huko Timnath-sera; ulio katika nchi ya vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.
Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, naye alikuwa na umri wa miaka mia moja na kumi.
Nao wakamzika katika mpaka wa urithi wake katika Timnath-heresi, katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, upande wa kaskazini wa mlima wa Gaashi.