Na Israeli waliosalia, katika hao makuhani, na Walawi, walikuwamo kote mijini mwa Yuda, kila mtu katika milki yake.
Yoshua 24:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Halafu Yoshua akawaruhusu watu waondoke; nao wakaenda kila mmoja kwake. Biblia Habari Njema - BHND Halafu Yoshua akawaruhusu watu waondoke; nao wakaenda kila mmoja kwake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Halafu Yoshua akawaruhusu watu waondoke; nao wakaenda kila mmoja kwake. Neno: Bibilia Takatifu Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe. Neno: Maandiko Matakatifu Basi Yoshua akawatuma watu kila mmoja aende katika urithi wake mwenyewe. BIBLIA KISWAHILI Basi Yoshua akawaruhusu watu, wakaenda zao, kila mtu kwenye urithi wake. |
Na Israeli waliosalia, katika hao makuhani, na Walawi, walikuwamo kote mijini mwa Yuda, kila mtu katika milki yake.
Hivyo hapana urithi wowote wa wana wa Israeli utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa wana wa Israeli watashikamana kila mtu na urithi wa kabila la baba zake.
Hivyo hapatakuwa na urithi wowote utakaotoka kabila hili kwenda kabila hili; kwa kuwa makabila ya wana wa Israeli yatashikamana kila mmoja na urithi wake mwenyewe.
Yoshua akawaambia watu wote, Tazama, jiwe hili litakuwa shahidi juu yetu; kwa maana limesikia maneno yote ya BWANA aliyotuambia, basi litakuwa shahidi juu yenu, msije mkamkana Mungu wenu.
Ikawa, baada ya hayo, Yoshua, mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, mwenye umri wa miaka mia moja na kumi.
Basi hapo Yoshua alipowapa watu ruhusa waende zao, wana wa Israeli wakaenda kila mtu kuuendea urithi wake, ili kuimiliki hiyo nchi.