Lakini Amazia hakutaka kusikia. Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda, huko Beth-shemeshi ulio wa Yuda.
Yoshua 19:38 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema - BHND Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yironi, Migdaleli, Horemu, Beth-anathi na Beth-shemeshi. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na tisa pamoja na vijiji vyake. Neno: Bibilia Takatifu Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake. Neno: Maandiko Matakatifu Ironi, Migdal-Eli, Horemu, Beth-Anathi na Beth-Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa na vijiji vyake. BIBLIA KISWAHILI Ironi, Migdal-eli, Horemu, Bethanathi na Beth-shemeshi; miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake. |
Lakini Amazia hakutaka kusikia. Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda, huko Beth-shemeshi ulio wa Yuda.
kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;
na mpaka ukafikia hadi Tabori, na Shahasuma na Beth-shemeshi; na mwisho wa mpaka wao ulikuwa katika mto wa Yordani; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Beth-shemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya, hao wenyeji wa Beth-shemeshi, na wenyeji wa Bethi-anathi, wakawatumikia kazi ya shokoa.