Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi.
Yoshua 18:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Zela, Ha-elefu, Yebusi, yaani Yerusalemu, Gibea na Kiriath-yearimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu waliyopewa watu wa kabila la Benyamini na koo zao. Biblia Habari Njema - BHND Zela, Ha-elefu, Yebusi, yaani Yerusalemu, Gibea na Kiriath-yearimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu waliyopewa watu wa kabila la Benyamini na koo zao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Zela, Ha-elefu, Yebusi, yaani Yerusalemu, Gibea na Kiriath-yearimu. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu waliyopewa watu wa kabila la Benyamini na koo zao. Neno: Bibilia Takatifu Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake. Neno: Maandiko Matakatifu Zela, Elefu, mji wa Wayebusi (yaani Yerusalemu), Gibea na Kiriathi; miji kumi na minne pamoja na vijiji vyake. Huu ndio uliokuwa urithi wa Benyamini kwa ajili ya koo zake. BIBLIA KISWAHILI na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao. |
Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi.
na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini;
Kisha mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu ili kupigana na Wayebusi, wenyeji wa nchi ile; nao wakamwambia Daudi, hutaingia humu kamwe; maana hata vipofu na viwete watakufukuzia mbali; huku wakidhania ya kuwa Daudi hawezi kuingia humo.
Naye Daudi alisema siku hiyo, Yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, na kuwapiga viwete, na hao vipofu, ambao roho yake Daudi inawachukia. Kwa sababu hii watu husema, Wako vipofu na viwete hawawezi kuingia nyumbani.
Hao ndio waliokuwa wakuu wa mbari za baba zao, katika vizazi vyao vyote, watu maarufu; na hao walikuwa wakikaa Yerusalemu.
wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.
Kimbieni mpate kuwa salama, enyi wana wa Benyamini; tokeni katika Yerusalemu, pigeni tarumbeta katika Tekoa, simamisheni ishara juu ya Beth-hakeremu; kwa maana mabaya yanachungulia toka kaskazini, na uharibifu mkuu.
Ee Israeli, umefanya dhambi tangu siku za Gibea; huko ndiko walikosimama; Je, vita juu ya wana wa uovu hakitawapata katika Gibea?
Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu;
Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake.
Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali popote kura itakapomwangukia mtu yeyote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama makabila ya baba zenu yalivyo.
Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.
kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;
kisha mpaka uliteremka hadi mwisho wa mlima ulio pale mkabala wa bonde la mwana wa Hinomu, lililo pale katika bonde la Warefai, upande wa kaskazini; nao ukateremkia mpaka bonde la Hinomu, hadi ubavuni mwa Myebusi upande wa kusini, kisha ukateremka hadi Enrogeli,
Kisha sehemu ya pili ilitokea kwa ajili ya Simeoni, maana, kwa ajili ya hilo kabila la wana wa Simeoni, kwa kufuata jamaa zao; na urithi wao ulikuwa katikati ya urithi wa wana wa Yuda.
Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa mji wa Yerusalemu; bali Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Benyamini ndani ya Yerusalemu hata hivi leo.
Lakini huyo mtu hakukubali kukaa usiku huo, ila akainuka, akaenda zake, akafika mkabala wa Yebusi (huo ndio Yerusalemu); nao walikuwako pamoja naye punda kadhaa waliotandikwa; suria wake naye alikuwa pamoja naye.
Sauli naye akaenda nyumbani kwake huko Gibea; na pamoja naye wakaenda kikosi cha watu, ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao.