Yoshua 14:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kwenda na kurudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote. Biblia Habari Njema - BHND Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini bado nina nguvu kama nilivyokuwa wakati ule Mose aliponituma. Hata sasa nina nguvu za kuweza kupigana vita au kufanya kazi nyingine yoyote. Neno: Bibilia Takatifu Bado nina nguvu kama siku ile Musa aliponituma; nina nguvu za kwenda vitani sasa kama nilivyokuwa wakati ule. Neno: Maandiko Matakatifu Bado ninazo nguvu kama siku ile Musa aliponituma. Bado ninazo nguvu za kwenda vitani sasa kama vile nilivyokuwa wakati ule. BIBLIA KISWAHILI Hata sasa mimi nina nguvu zangu hivi leo kama nilivyokuwa siku hiyo Musa aliyonituma; kama nguvu zangu zilivyokuwa wakati huo, na nguvu zangu ndivyo zilivyo sasa, kwa vita na kwa kwenda na kurudi. |
Miaka ya maisha yetu ni sabini, Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini; Tena kiburi chake ni taabu na ubatili, Maana wakati unapita upesi nasi kutokomea punde.
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Akawaambia, Mimi leo ni mwenye miaka mia moja na ishirini; siwezi tena kutoka na kuingia, na BWANA ameniambia, Hutavuka mto huu Yordani.
Makomeo yako yatakuwa ya chuma na shaba; Na kadiri ya siku zako ndivyo zitakavyokuwa nguvu zako.
Musa alikuwa mtu wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; jicho lake halikupofuka, wala nguvu za mwili wake hazikupunguka.
Sasa basi, angalia, yeye BWANA ameniweka hai, kama alivyosema, miaka hii arubaini na mitano, tangu wakati huo BWANA alipomwambia Musa neno hilo, wakati Israeli walipokuwa wanapitia jangwani; na sasa tazama, hivi leo nimetimiza umri wa miaka themanini na mitano.