na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hadi Nebo na Baal-meoni;
Yoshua 13:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ilikuwa pia pamoja na Heshboni na miji yake yote iliyo katika sehemu tambarare: Yaani Diboni, Bamoth-baali, Beth-baal-meoni, Biblia Habari Njema - BHND Ilikuwa pia pamoja na Heshboni na miji yake yote iliyo katika sehemu tambarare: Yaani Diboni, Bamoth-baali, Beth-baal-meoni, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ilikuwa pia pamoja na Heshboni na miji yake yote iliyo katika sehemu tambarare: yaani Diboni, Bamoth-baali, Beth-baal-meoni, Neno: Bibilia Takatifu hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, Neno: Maandiko Matakatifu hadi Heshboni na miji yake yote kwenye uwanda wa juu, ikijumlishwa miji ya Diboni, Bamoth-Baali, Beth-Baal-Meoni, BIBLIA KISWAHILI na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni; |
na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hadi Nebo na Baal-meoni;
Na kuhusu habari za vijiji na mashamba yake; wengine wa wana wa Yuda walikuwa wakikaa Kiriath-arba na vijiji vyake, na katika Diboni na vijiji vyake, na Yekabzeeli na vijiji vyake;
Ee binti ukaaye Diboni, Shuka toka utukufu wako, ukae katika kiu; Maana atekaye Moabu amepanda juu yako, Ameziharibu ngome zako.
Naye mwenye kuteka nyara atakuja juu ya kila mji, wala hakuna mji utakaookoka; bonde nalo litaangamia, nayo nchi tambarare itaharibiwa; kama BWANA alivyosema.
basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu,
Kwa kuwa Heshboni ulikuwa ni mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akipigana na mfalme wa Moabu wa mbele, na kumpokonya nchi yake yote mkononi mwake, mpaka mto wa Arnoni.
Tumewapigia mishale; Heshboni umepotea mpaka Diboni, Nasi tumeharibu mpaka Nofa, Ifikiayo Medeba.
Ikawa asubuhi Balaki akamchukua Balaamu, akampandisha hadi Bamoth-baali; na kutoka huko aliweza kuwaona baadhi ya Waisraeli hadi pande zao za mwisho.
na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine.
Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba;
Kwa kuwa Musa alikuwa amekwisha kuwapa urithi hayo makabila mawili na nusu, ng'ambo ya pili ya Yordani; lakini hakuwapa Walawi urithi wowote kati yao.
Kwa maana Walawi hawana fungu kati yenu; Kwa kuwa huo ukuhani wa BWANA ndio urithi wao; tena Gadi, na Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, wamekwisha pata urithi wao ng'ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki, ambao walipewa na Musa, mtumishi wa BWANA.
Wakati Israeli walipokuwa wakikaa Heshboni na miji yake, na katika Aroeri na miji yake, na katika miji hiyo yote iliyo huko kando ya Arnoni, muda wa miaka mia tatu; mbona hamkuikomboa wakati huo?