Yohana 8:56 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Abrahamu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi.” Biblia Habari Njema - BHND Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Abrahamu, baba yenu, alishangilia aione siku yangu; naye aliiona, akafurahi.” Neno: Bibilia Takatifu Baba yenu Ibrahimu alishangilia kwamba angeiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.” Neno: Maandiko Matakatifu Baba yenu Ibrahimu alishangilia kwamba angaliiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.” BIBLIA KISWAHILI Abrahamu, baba yenu, alishangilia kwa vile atakavyoiona siku yangu; naye akaiona, akafurahi. |
Kwa maana, amin, nawaambia, Manabii wengi na wenye haki walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi, wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi, wasiyasikie.
Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.
Yesu akawajibu, Niliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia.
Najua ya kuwa ninyi ni uzao wa Abrahamu lakini mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halimo ndani yenu.
Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Abrahamu! Yesu akawaambia, Kama mngekuwa watoto wa Abrahamu, mngezitenda kazi zake Abrahamu.
Hawa wote wakafa katika imani, walikuwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia, na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.