Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Yohana 7:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.” Biblia Habari Njema - BHND Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini mimi namjua kwa sababu nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma.” Neno: Bibilia Takatifu Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.” Neno: Maandiko Matakatifu Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.” BIBLIA KISWAHILI Mimi namjua, kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye aliyenituma. |
Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu; wala hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia.
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua.
kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Yesu, huku akijua ya kuwa Baba amempa vyote mikononi mwake, na ya kuwa alitoka kwa Mungu naye anakwenda kwa Mungu,
Wala ninyi hamkumjua; lakini mimi namjua. Nikisema ya kwamba simjui, nitakuwa mwongo kama ninyi; lakini namjua, na neno lake nilishika.
(na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena tunashuhudia, na kuwahubiria ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye.