Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Yohana 7:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hapo watu wakamjibu, “Una pepo wewe! Nani anataka kukuua?” Biblia Habari Njema - BHND Hapo watu wakamjibu, “Una pepo wewe! Nani anataka kukuua?” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hapo watu wakamjibu, “Una pepo wewe! Nani anataka kukuua?” Neno: Bibilia Takatifu Ule umati wa watu wakamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?” Neno: Maandiko Matakatifu Ule umati wa watu ukamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?” BIBLIA KISWAHILI Mkutano wakajibu, Ama! Una pepo! Ni nani anayetafuta kukuua? |
Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake?
Lakini Mafarisayo waliposikia, walisema, Huyu hatoi pepo, ila kwa Beelzebuli mkuu wa pepo.
Wayahudi wakajibu, wakamwambia, Je! Sisi hatusemi vema ya kwamba wewe u Msamaria, nawe una pepo?
Yesu akajibu, Mimi sina pepo; lakini mimi namheshimu Baba yangu, na ninyi mwanivunjia heshima yangu.
Basi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumeng'amua ya kuwa una pepo. Abrahamu amekufa, na manabii wamekufa; nawe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti milele.
Alipokuwa akijitetea hivi, Festo akasema kwa sauti kuu, Paulo, una wazimu, kusoma kwako kwingi kumekugeuza akili.