Yohana 6:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope!” Biblia Habari Njema - BHND Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope!” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope!” Neno: Bibilia Takatifu Lakini Isa akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” Neno: Maandiko Matakatifu Lakini Isa akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.” BIBLIA KISWAHILI Naye akawaambia, Ni mimi, msiogope. |
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Usiogope, Yakobo uliye mdudu, nanyi watu wa Israeli; mimi nitakusaidia, asema BWANA, na mkombozi wako ni Mtakatifu wa Israeli.
Msiogope wala msifanye hofu; je! Sikukuambia haya zamani na kuyatangaza? Na ninyi ni mashahidi wangu. Je! Yuko Mungu zaidi yangu mimi? Hakika hapana Mwamba; mimi sijui mwingine.
Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulubiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.
kwa kuwa wote walimwona, wakafadhaika. Mara akasema nao, akawaambia, Changamkeni; ni mimi, msiogope.
Basi wakavuta makasia kadiri ya maili tatu nne, wakamwona Yesu anakwenda juu ya bahari na kuikaribia mashua; wakaogopa.
Basi wakataka kumpokea katika mashua; na mara hiyo mashua ikaifikia nchi waliyokuwa wakiiendea.