Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Yohana 17:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao. Biblia Habari Njema - BHND “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Siwaombei hao tu, bali nawaombea pia wote watakaoamini kutokana na ujumbe wao. Neno: Bibilia Takatifu “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao, Neno: Maandiko Matakatifu “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao BIBLIA KISWAHILI Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. |
Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja.
Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma.
Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapatao elfu tatu.
Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya wanaume ikawa kama elfu tano.
ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.