Lakini ninyi, enyi milima ya Israeli, mtachipuza matawi yenu na kuwapa watu wangu Israeli matunda yenu; maana wako karibu kuja.
Yoeli 2:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mahali pa kupuria patajaa nafaka, mashinikizo yatafurika divai na mafuta. Biblia Habari Njema - BHND Mahali pa kupuria patajaa nafaka, mashinikizo yatafurika divai na mafuta. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mahali pa kupuria patajaa nafaka, mashinikizo yatafurika divai na mafuta. Neno: Bibilia Takatifu Sakafu za kupuria zitajaa nafaka, mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. Neno: Maandiko Matakatifu Sakafu za kupuria zitajaa nafaka, mapipa yatafurika mvinyo mpya na mafuta. BIBLIA KISWAHILI Na sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai na mafuta. |
Lakini ninyi, enyi milima ya Israeli, mtachipuza matawi yenu na kuwapa watu wangu Israeli matunda yenu; maana wako karibu kuja.
Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana.
Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya BWANA, na kulinywesha bonde la Shitimu.
Nanyi mtakula akiba ya zamani mliyoiweka siku nyingi, tena hayo ya zamani mtayatoa, ili myaweke yaliyo mapya.
Angalieni, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo huyo alimaye atamfikia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.